Twasifu Jina Lako

Artist: Congress MusicFactory
Produced By: Congress MusicFactory
Album: Twakuabudu

[Pambio]
Bwana mungu ameinuliwa
Mfalme wa wafalme ametukuka
Hakuna mwingine ameinuliwa
Twasifu jina lako

[Ubeti wa 1]
Uwezo wote ni wako bwana
Neno lako ni uzima tena kweli
Maisha yetu twatoa kwako bwana
Twasifu jina lako

[Ubeti wa 2]
Bwana yesu twainua jina lako
Wema na upendo wako twatangaza
Kwashukrani twainama na kuabudu
Twasifu jina lako