Daima Na Kuinua

Artist: Congress MusicFactory
Produced By: Congress MusicFactory
Album: Twakuabudu

[Ubeti wa 1]

Nguvu yangu, ngao yangu,
Imani yangu, nakuamini wee,
Furaha yangu, ficho langu,

[Pambio ya 1]

Milele nakuinua, bwana
Nakuabudu nakuabudu,
Nakuinua bwana nakuabudu,
Nakuabudu.

[Ubeti wa 2]

Kweli yangu, uniongoza,
Mwenye-enzi ninaye sujudu.
Nakupasifa ,na kuheshimu

[Pambio ya 2]

Milele nakuinua bwana,
Nakuabudu nakuabudu,
Nakuinia bwana nakuabudu,
Nakuabudu.

[Ombi]

Mambo mengi tunayoyafanya yataisha ibada yako itadumu milele amina, lakini tutamuabudu milele unapomuabudu unajizoesha tabia ya milele. Mambo yanayojaza mawazo yetu sasa yatakoma lakini ibada yako itadumu milele, amina, daima tutainua mioyo yetu kwake milele, unapomuabudu mungu ni kama unaikana dunia, unakana wakati , unakana kifo na unakana hali ya mauti, mambo mengine tayari ni ya milele katika uzoevu wangu wa kibinadamu na ibada yako itaendelea milele.

[Pambio ya 3] Milele twakuinua bwana,
Twakuabudu twakuabudu,
Twakuinia bwana twakuabudu,
Twakuabudu.

[Pambio ya 4] Twakuenzi bwana,
Twakuabudu, twakuabudu
Twakuinua bwana, twakuabudu
Twakuabudu.