Nainua Mikono Yangu Kwako (Ombi)

Artist: Congress MusicFactory
Produced By: Congress MusicFactory
Album: Twakuabudu

Hebu tuinue mikono yetu takatifu kwa bwana, amina? Baba tunainua mikono yetu kwako wewe, kila mmoja wetu. Ndugu yangu anainua mikono yake karibu nami. Dada yangu anainua mikono yake karibu nami na ninawaza juu ya mstari mrefu wa uzuri na heshima na utiifu. Uzuri wa utiifu ambao ulituleta mahali hapa. Nainua mikono nikiwaza juu ya dhabihu ya ndugu na dada zetu walio tutangulia, ambao walikabiliana na gathabu za adui na kutoa maisha yao, na kumwaga damu ili kuunda njia hii ya nuru tunayotembelea. Na ninawakumbuka ninapoinua mikono yangu. Nakumbuka kile kilichoniumba kunifanya nilivyo leo. Maneno na milio na uamuzi na dhabihu na utiifu, miaka baada ya miaka, kizazi baada ya kizazi ilioandaa njia hii tunayosimama kwayo.

Na natoa shukrani kwako wewe kwa ajili ya uthabiti wako na uaminifu na uamuzi wako wa kujenga na kuimarisha na kuhimiza na kutuma roho wako ndani ya mioyo ya wanadamu. Tunashukuru.
Tunashukuru kwa sababu ya kutupa uzima. Tunashukuru kwa sababu mioyo yetu inainuka kwa kuimba. Nashukuru kwa sababu ya kuketi kati ya ndugu zangu. Nuru imeingia ndani ya mawazo yangu, na nafsi yangu na roho yangu. Nikiskia sauti ya viongozi wangu. Nikiskia matamshi ya roho mtakatifu na kutazama uso wa mungu imekua ya kipekee na ya heshima na ya kupendeza. Nakutazama wewe. Yanifanya kuwa mtu bora. Kukuangalia tu wewe baba, kutazama ndani ya moyo wako kunanifanya kua mtu bora. Kunanifanya kua mtu bora na ninashukuru.

Asante kwa kunihifadhi. Asante kwa kuniongoza. Asante kwa kuueka mkono wako juu yangu. Asante kwa kunipatia uzima. Asante kwa kunifundisha kwa subira. Asante kwa kuniongoza kutoka kwa ubatili na kunileta kwa hekima. Asante kwa kuniondoa kutoka kwa udhaifu na kunipatia nguvu. Asante kwa kuondoa shaka yangu na kunipa imani. Asante kwa kunitoa kwenye mauti na kunipa uhai wa kipekee. Asante kwa kunitoa kwenye upweke na kuniweka kati ya watu hawa wa ajabu, watu wa kipekee. Asante kwa kuitoa kwenye kutangatanga na kunipatia safari. Ninakushukuru. Ninakushukuru mungu. Asante bwana. Asante kwa kuniumba. Asante kwa kunipa uhai. Asante kwa kuniweka wakfu. Asante kwa kunituma. Asante kwa kuniteua. Asante kwa kuniongoza. Asante! Asante! Asante! Asante! Asante kwa vita vyote. Asante kwa ajili ya kila ushindi, kila jaribu. Asante kwa sehemu ngumu. Asante kwa sehemu rahisi. Asante kwa ajili ya kila kitu, kila saa, kila mda, kila mahali. Mahali ambapo mkono wako uligusa maisha yangu. Ninasema asante. Asante mungu! Asante.