Njia Hii (Ombi)

Artist: Congress MusicFactory
Produced By: Congress MusicFactory
Album: Twakuabudu

Nawe utasikia sauti nyuma yako ikisema, “njia ni hii. Ifuateni.” Hebu sauti hio iwe katika nyumba zetu na katika ndoa zetu. Nataka watu wote wasikie sauti hio, sauti nyuma yako ikikuongoza ikisema, “njia ni hii. Ifuateni.”

Hebu nisikie sauti hio katika maisha yangu kupitia zamu zote na uramazaji wakuja kwako ambapo hakuna mwongozo kwa mtu yeyote. “njia ni hii. Ifuateni.” Tunaskia sauti wazi ya mungu, sahihi. Wazi wakati wa mwangaza na tunasema mungu hebu iwe uwazi na ya kuangaza ndani ya mioyo yetu. Tupe uwezo wa kupambanua kwa uwazi na kwa nguvu kile ambacho ni cha mungu na kile ambacho sio cha mungu. Kile cha haki, kile kibaya na kisicho takatifu. Kilicho cha ukweli na kile cha uwongo. Tuwezeshe kusikia sauti nyuma yetu ikisema, “njia ni hii. Ifuateni.”

Tupe mwelekeo kutoka mbinguni na mwongozo wazi kutoka mahali pa juu pa mamlaka, juu ya kuchanganyikiwa kwa dunia hii. Juu ya udanganyifu na falsafa yake, juu ya uchafu wake na uongozi wake. “njia ni hii. Ifuateni.” Kutoka muda huu kutoka wakati hadi mwisho wa wakati katika hali zote ambazo utaleta kwa nguvu zako hapa duniani katikati ya hayo. Tutengenezee njia wazi ikituelekeza moja kwa moja kwenye kiti chako cha enzi.

Tupe imani ili kueka miguu yetu katika njia tunaposikia mioyoni mwetu, “njia ni hii. Ifuateni. Ifuateni. Ifuateni. Ifuateni.”