Njia Hii

Artist: Congress MusicFactory
Produced By: Congress MusicFactory
Album: Twakuabudu

[Ubeti wa 1]
Hatuthamini ya kale
Atuongoza pahali
Hakuna aliyefika
Kuna ishara hewani
Twahisi atenda jambo jipya

[Pambio Tangulizi 1]
Mioyo iliyo tupu,
Imepata utele
Njia ya utimilifu,
Ya nia yake iwazi

Hifadhi kapatikana,
Neema mpya yashuka
nguvu hekima ya utimizo,
wa lengo la bwana.

[Pambio Tangulizi 2]
Eeh bwana tuma sauti,
Kusanya wateule
Pamoja twainuka twaangaza,
Kwako nuru yetu yajaa

[Pambio]
Giza limetanda,
Hakuna ufahamu
Twazingirwa nazo hali,
Za kuyeyusha mioyo

Tukati ya wenye hekima, wanaoinuka
Twaongoza mataifa,
Tuwafungue macho x2

[Kumalizia]
Hatuthamini ya kale
Atuongoza pahali
Hakuna aliyefika
Uwepo wake wahakikisha
Njia hii itatembelewa
Na wengi zaidi…….