Twakuabudu

Artist: Congress MusicFactory
Produced By: Congress MusicFactory
Album: Twakuabudu

[Ombi]

Twakuabudu,twakubariki na tunainua jina lako. Tunainua mikono zetu kwako kama vile mababa zetu walivyofanya,wazee wetu wa tangu zamani. Walivyoinua mikono yao takatifu kwako mungu mwenye enzi na kama vile ndugu yangu Habakkuki alivyosema miaka na miaka mingi iliyopita:
“Nitafurahi, nitafurahia. Ewe Bwana mwenye enzi, ni nguvu yangu ”Wewe ndiye nguvu ya ndugu yangu.”Wewe huwezesha miguu yangu kame kulungu.Unanitia nguvu, na kuniinua juu

Kwa hivyo kuanzia wakati huu twasonga mbele na kuyainua macho yetu, twainuka nakutembea ndani ya utukufu ulio ndani yako na tunabariki jina lako takatifu

Ahsante kwa neno lako. Ahsante kwa kutufundisha. Ahsante kwa kutufunza. Hebu neno lako likaangukie udongo ulio na utajiri ndani ya mioyo yetu, hebu mizizi yake iingie ndani na kuzalisha katika ndani zangu wote. Watakatifu wako wote, mara thelathini, mara sitini na mara mia moja katika mambo ya Mungu
Ahsante Mungu.Tunakubariki.Amina.Amina

[Pambio]

Twakubariki,
pokea sifa,
umetukuka milele,

Mungu Mkuu,
Nguvu Yetu,
Twakuabudu Milele